Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Abdulkadir Kaita, ameviambia vyombo vya habari kuwa baadhi ya mashamba ya nyanya yaliyopo kwenye majimbo ya Kano, Jigawa, Plateau, Katsina na
Kaduna, yameathiriwa na mdudu aitwaye Tuta Absoluta aliyeharibu nyanya kwenye mashamba yote na kupelekea upungufu mkubwa wa zao hilo.
Kaita alidai kuwa uzalishaji utaanza tena katika msimu ujao. Dangote Group, kampuni ya Dangote ilianzisha kiwanda cha kusindika nyanya kwa gharama ya dola milioni 20 katika jimbo la Kano mapema mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment