Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Madee, amesema ndoa nyingi za vijana zinavunjika kutokana na vijana wengi kukurupuka kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Madee2
Akizungumza katika kipindi cha Uhondo cha EFM, Madee amesema yeye anataka kuwa mfano wa kuigwa pindi atakapoingia kwenye maisha ya ndoa.
“Time ikifika nitaoa tu kwa sababu hivi vitu havihitaji haraka, leo nimchukue mtoto wa watu alafu baada ya miezi kadhaa nimrudishe kwao nitakuwa nimeitukana familia yao na yangu pia,” alisema Madee. “So wale wote ambao, wanakurupuka tunaona mwisho wao ni kuachana au kugombana kila siku. So mimi nasubiria time yangu, nikishaoa ndo nimemaliza, mimi nataka kuja kuwa mfano kwa wengine,”
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video ya wimbo wake ‘Migulu Pande’, ni baba wa mtoto mmoja aitwae Saida.

Advertisement

0 comments:

Post a Comment

 
Top